Nyoka ni mnyama mdogo lakini anayeogopwa hata na majambazi wakubwa. Adui wa dirishani alipogeuka kumwangalia Murphy, alimwangalia pia mwenzake na kucheka bila Murphy kujua kilichofanya wafurahi. Ghafla, kuna kitu kilitokea! Nyoka mkubwa aina ya swila aliruka toka dirishani na kuanguka katika mabega ya yule adui. Adui aliruka kwa woga na kuanguka chini … halafu yakatokea maajabu! Bunduki ilifyatuka kutoka nje, ikaripuka kwa sauti ya juu, walinzi wote wa Murphy wakaruka na kuanguka chini shaghalabaghala, na kufa papo kwa papo!

Related Quotes