Murphy alichanganyikiwa. Hakujua nini kilitokea na kwa nini. Ila, ghafla, alipotupa macho kushoto aliona kitu. Joka kubwa lilitambaa, ingawa kwa shida, kwa sababu ya sakafu, na kumfuata kummaliza. Murphy alijua joka hata angefanya vipi, hakuwa na uwezo wa kujikinga. Alipotaka kupiga kelele ili walinzi wa nje waje, Murphy alishindwa. Nyuma ya joka – katika mkia – kuna kitu kiling’aa, kikamshangaza! Muujiza ulimtokea Murphy lakini kitu kikamwambia aite walinzi wa nje ili waje wamuue yule nyoka. Lakini kabla hajapiga kelele, alisikia sauti; si ya mwanamume. Ya mwanamke!

Related Quotes