Lakini, akiendelea kuwaza na kuangaza, ghafla Murphy aliona kitu kama gari likiwa limesimama kwa mbali. Alisimama na kupata hamu ya kujua. Murphy alianza tena kutembea, lakini sasa akiifuata ile gari, halafu akaongeza mwendo na kukimbia; macho yote yakiwa mbele! Alipofika, karibu na gari ile, hakuminya kifyatulio kumpiga mtu risasi. Alijenga tabasamu na kuongeza mwendo. Gari ilikuwa Ferrari Testarrosa ya Lisa Madrazo Graciano!

Related Quotes

Murphy. Sina mbinu zozote za kujikinga kama unavyojua; mbali na mafunzo ya FBI. Baada ya kumrusha nyoka wa Lisa nywele zilinisisimka. Wazo la kukimbia likaja ghafla. Kukimbia hata hivyo nikashindwa kwa kuhofu huenda wangeniona. Hivyo, nikarudi nyuma ya nyumba na kupanda mti na kujificha huko. Bunduki zilipolia, nilijua wamekuua. Ila kitu kimoja kikanishangaza: mashambulizi hayakuonekana kukoma. Kitu hicho kikanipa nguvu kwamba huenda hujafa na ulikuwa ukipambana nao. Kimya kilipotokea nilijua umewashinda nguvu, kitu ambacho kumbe kilikuwa kweli. Nilipokutafuta baadaye lakini bila kukuona kutokana na kukurukakara za maadui niliamua kwenda katika gari ili nije na gari kama mgeni, nikitegemea waniruhusu kuingia ili nipate hakika kama wamekuua au bado uko hai. Wasingenifanya chochote. Kimaajabu, niliposhuka katika mti ili nikimbie katika gari, niliona gari ikija kwa kasi. Kuangalia vizuri nikakuta ni Ferrari, halafu nikashangaa nani anaendesha gari ya Lisa!”
Murphy alitabasamu tena na kuendelea kusikiliza.
“Sijui moyo wangu ulikuwaje. Sikuogopa tena! Badala yake nilikaza mwendo na kuendelea kuifuata huku nikipata wazo hapohapo kwamba mtu aliyekuwemo akiendesha hakuwa adui. Adui angeingia katika gari na kunisubiri aniteke nyara.” Debbie alitulia.
“Ulihisi ni mimi?” Murphy aliuliza.
“Nilihisi ni mtu tu mwema amekuja kunisaidia ... au mwizi wa gari. Hata hivyo, baadaye nilijua ni wewe na furaha yangu yote ilirudi.
Enock Maregesi
aliveautomobilebunduki