Falaki maana yake ni kundi la nyota na sayari ikiwemo dunia. Falaki yetu inaitwa Njiamaziwa, ‘the Milky Way galaxy’, yenye mabilioni ya mifumo ya jua ukiwemo wa kwetu. Mungu alisimamisha jua katika falaki ya Njiamaziwa kwa ajili ya Yoshua, ili apate muda wa kutosha kuwashinda maadui zake – wanajeshi wa mataifa matano. Kila mtu alishangaa sana kipindi hicho. Kila mtu anashangaa sana kipindi hiki. Mungu akikubariki watu watasema wewe ni mchawi. Hawatajua nini kilitokea. Kwani kwa Mungu hakuna kinachoshindikana. Mungu aliweza kutenda miujiza kwa ajili ya Yoshua, na kwa ajili ya wana wa Israeli huko Gibeoni na huko Aiyaloni, anaweza kutenda miujiza kwa ajili yako popote pale ulipo. Mungu anachotaka kutoka kwako ni imani ya kweli juu yake, kwa mwili na kwa roho yako yote.
— Enock Maregesi
aijalonaiyalonibillions