Sayari yetu hujulikana kama Dunia na jua letu hujulikana kama Sol. Dunia imo ndani ya mfumo wa jua wa Sol. Mfumo wa jua wa Sol umo ndani ya mfumo wa jua wa Sol Sector au Solar Interstellar Neighborhood, kwenye wenzo wa Orion wa falaki ya Njiamaziwa, wenye mifumo ya jua zaidi ya 40 ikiwemo Alpha Centauri, Nemesis, Procyon na Sirius. Solar Interstellar Neighborhood imo ndani ya falaki ya Njiamaziwa yenye nyenzo nne zinazozunguka kwa pamoja na falaki nzima. Falaki ya Njiamaziwa imo ndani ya kishada (‘cluster’) chenye zaidi ya falaki 55 ikiwemo Andromeda, Leo A, M32 na Triangulum, kinachojulikanacho kama ‘the Local Galactic Group’. ‘The Local Galactic Group’ imo ndani ya mfumo wa kishada kikubwa zaidi kiitwacho Virgo Supercluster, chenye makundi zaidi ya 100 ya falaki. Virgo Supercluster imo ndani ya mfumo mwingine mkubwa zaidi wa vishada uitwao Laniakea (Local Supercluster) wenye vishada zaidi ya 500 vya falaki. Hapo ndipo mwisho wa ulimwengu wetu unaoweza kuonwa na wanasayansi wetu. Kutoka duniani mpaka Laniakea ni umbali wa kilometa bilioni trilioni 250, miaka bilioni 13.8 iliyopita.
— Enock Maregesi
13-8-billion-years-ago250-billion-trillion-kilometers55-galaxies