Kama kuna swali maarufu kuliko yote katika kitabu cha 'Kolonia Santita' ni "Кто Вы, где Вы от, и почему Вы в Москве?" lililoulizwa na товарищи (Komredi) Anatoly-Chaika, baada ya kumfikisha Murphy katika 'dacha' ya Kolonia Santita ya Yugo Zapadnaya. Murphy hakumwelewa Chaika. Lakini mwenzake na Chaika (Vladimir) alipouliza kwa tafsiri, "Wewe ni nani, unatoka wapi, na unafanya nini Moscow?" Murphy alimwelewa na kucheka akiwa amenuna. Bila swali hilo asingeokoka.

Related Quotes