Mungu ni mtakatifu na kwa maana hiyo hatendi dhambi. Hivyo, hauwi wala hatesi. Tunajiua na kujitesa wenyewe. Ametupa hiari ya kuchagua mema au mabaya. Lakini anamtumia Shetani kama wakala wake wa kutoa adhabu kwa binadamu pale tunapoenenda sawasawa na machukizo yake. Damu ina nguvu kuliko Shetani na ina nguvu kuliko kuzimu. Unapojifunika kwa damu ya Mwanakondoo, Shetani hataweza kukuona. Hivyo, hataweza kukudhuru. Lakini usipojifunika kwa damu ya Mwanakondoo, Shetani atakuona. Hivyo, atakudhuru. Atakudhuru kwa sababu Mungu atakuwa ameruhusu akudhuru, kwa sababu ya uhuru wa kuchagua mema au mabaya aliotupatia, ijapokuwa ana uwezo wa kuzuia asikudhuru. Kwa mtindo huo Mungu anakuwa ametoa adhabu kwa binadamu.
— Enock Maregesi
abhorrenceadhabuagent