Nguvu za hasi ni mawazo mabaya, na nguvu za chanya ni mawazo mazuri. Nguvu za hasi ni Shetani, kwa vile Shetani ndiye anayeleta mabaya. Nguvu za chanya ni Mungu, kwa vile Mungu ndiye anayeleta mazuri. Katika dunia hii utapambana na Shetani lakini hutamshinda, kwani hapa ndipo anapotawala. Pambana na Shetani katika dunia ya kiroho, kwa maana ya maombi na utiifu kamili kwa Mwenyezi Mungu, kama unataka kuzishinda nguvu zake.