Ndani ya gruneti kuna vitu kumi vyenye uwezo na visivyokuwa na uwezo wa kulipuka kama vile pini, mtaimbo, springi ya mtaimbo, tundu la kuingizia baruti, baruti, fataki, fyuzi, utambi, wenzo na ganda la chuma la pingili kama vipande vya risasi. Pini inapochomolewa, na bomu kurushwa kuelekea kwenye shabaha au kuelekea sehemu nyingine yoyote, wenzo wa usalama huchomoka pia na kuachana na bomu moja kwa moja. Wenzo wa usalama unapochomoka huruhusu mtaimbo ugonge fataki ya kuwashia fyuzi kwa nguvu na kasi kubwa. Fyuzi itawaka kwa sekunde nne kabla ya kuwasha utambi, ambao utawasha baruti ndani ya sekunde moja, kabla ya baruti kulipuka – na kusambaza vipande vya bomu katika kila sehemu ya shabaha.

Related Quotes