Mungu hatakubali kuwa na mtu katika ufalme wake ambaye hatakubali kutawaliwa naye. Usikubali kutawaliwa na Ibilisi, kubali kutawaliwa na Mungu. Ni jukumu letu kuanza kuishi sasa kama vile tutakavyoishi mbinguni. Shetani anataka uwe na hekima ya duniani ili akupumbaze. Lakini hofu ya Mungu ndiyo msingi wa hekima ya kweli. Ukitaka asikupumbaze, pokea Roho ya Mungu kwa kubatizwa. Ukiipokea Roho ya Mungu utajua mambo ya Mungu, ambayo dunia haiwezi kujua.

Related Quotes

Mungu alikuumba miaka mingi kabla hujazaliwa. Ndani ya roho yako kulikuwa na mpango mkuu wa Mungu juu ya maisha yako katika kipindi chote utakachokuwa hai, na katika kipindi chote utakachokuwa mfu. Lakini Shetani katika mji wa angani unaosemekana kuzuia majibu ya maombi ya Danieli ya siku ishirini na moja, kutoka mbinguni kuja duniani, uitwao Sadiki, wenye mashetani wenye nguvu kuliko mashetani wote katika ufalme wa giza, akaizuia roho hiyo kisha akaiwekea mpango mkuu wa Shetani juu ya maisha yako ili umtumikie yeye badala ya kumtumikia Mwenyezi Mungu.

Kwa mfano, Mungu alipanga uzaliwe mkoani Arusha. Halafu akapanga mke au mume wako azaliwe mkoani Mwanza. Mkoani Arusha Mungu alipanga uwe mwinjilisti wa vitabu, wakati mkoani Mwanza alipanga mke au mume wako awe mwimbaji wa nyimbo za injili. Katika mikoa yote miwili Mungu alishatuma malaika wema wa kuwasaidia katika mipango mikuu ya maisha yenu na kuwaepusha na hila zote za adui.

Lakini badala ya kuzaliwa Arusha au Mwanza Shetani ataziprogramu roho zenu upya ili wa Arusha azaliwe Dodoma au Mara au Venezuela na wa Mwanza azaliwe Lindi au Kagera au Mombasa, ambapo hakutakuwa na malaika wema wa kuwasaidia. Badala ya kuwa mwinjilisti wa vitabu, Shetani atakufanya uwe jambazi; na badala ya kuwa mwimbaji wa nyimbo za injili, Shetani atakufanya uwe mwanamuziki.

Ndiyo maana wakati mwingine ni vizuri kuhama sehemu unapoishi na kwenda kuishi sehemu nyingine, ambapo kwa kusaidiana na malaika wako wa mwanzo ambaye Mungu alikupangia kabla hujazaliwa, utafanikiwa katika maisha yako, kama alivyofanya Ibrahimu.

Watu wengi wanaishi maisha ambayo si ya kwao. Kukomboa kile ambacho Mungu alikipanga ndani ya roho yako kabla hujazaliwa, na kabla roho yako haijazuiwa na mashetani wa angani, kuwa karibu na Mwenyezi Mungu. Kwa Mungu hakuna siri, atakufunulia tu.
โ€” Enock Maregesi
alivecelestial-citydaniel-prayers
๐ŸŽฏ๐Ÿ“–๐ŸŽฏ๐Ÿ’ญ๐ŸŒŸ