Kilometa mbili na ushei kidogo kutoka katika sanamu la Yesu Mtoto liitwalo Niñopa, katika Kanisa la Parokia ya Manispaa ya Xochimilco ('Sochimiliko') la Iglesia de San Bernardino de Siena, Mexico City, kulikuwa na nyumba ndogo ya siri ('safe house') ya Kolonia Santita iliyojengwa bila uzio wa ukuta au seng’enge isipokuwa miti iliyopandwa kuizunguka bila mpangilio wowote. Ndani ya nyumba hiyo Mpelelezi Maarufu Duniani John Murphy alikuwa akiteswa na magaidi kumi na mbili; waliokuwa wakiendelea kushangaa jinsi alivyookoka katika ajali ya ndege iliyoua watu zaidi ya mia tatu huko Uholanzi, na jinsi alivyoweza kuingia katika ofisi ya siri ya Panthera Tigrisi, kitu kilichomchanganya akili Tigrisi na makompade wote wa Kolonia Santita duniani kote. Bila Mtoto wa Rais wa Meksiko Debbie Patrocinio Abrego, na mwanasesere wa nyoka wa Mtoto wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Lisa Madrazo Graciano, John Murphy angeanguka.

Related Quotes

Murphy. Sina mbinu zozote za kujikinga kama unavyojua; mbali na mafunzo ya FBI. Baada ya kumrusha nyoka wa Lisa nywele zilinisisimka. Wazo la kukimbia likaja ghafla. Kukimbia hata hivyo nikashindwa kwa kuhofu huenda wangeniona. Hivyo, nikarudi nyuma ya nyumba na kupanda mti na kujificha huko. Bunduki zilipolia, nilijua wamekuua. Ila kitu kimoja kikanishangaza: mashambulizi hayakuonekana kukoma. Kitu hicho kikanipa nguvu kwamba huenda hujafa na ulikuwa ukipambana nao. Kimya kilipotokea nilijua umewashinda nguvu, kitu ambacho kumbe kilikuwa kweli. Nilipokutafuta baadaye lakini bila kukuona kutokana na kukurukakara za maadui niliamua kwenda katika gari ili nije na gari kama mgeni, nikitegemea waniruhusu kuingia ili nipate hakika kama wamekuua au bado uko hai. Wasingenifanya chochote. Kimaajabu, niliposhuka katika mti ili nikimbie katika gari, niliona gari ikija kwa kasi. Kuangalia vizuri nikakuta ni Ferrari, halafu nikashangaa nani anaendesha gari ya Lisa!”
Murphy alitabasamu tena na kuendelea kusikiliza.
“Sijui moyo wangu ulikuwaje. Sikuogopa tena! Badala yake nilikaza mwendo na kuendelea kuifuata huku nikipata wazo hapohapo kwamba mtu aliyekuwemo akiendesha hakuwa adui. Adui angeingia katika gari na kunisubiri aniteke nyara.” Debbie alitulia.
“Ulihisi ni mimi?” Murphy aliuliza.
“Nilihisi ni mtu tu mwema amekuja kunisaidia ... au mwizi wa gari. Hata hivyo, baadaye nilijua ni wewe na furaha yangu yote ilirudi.
Enock Maregesi
aliveautomobilebunduki