Kwa vile hatasamehewa, Shetani hatawasamehe wanadamu. Atahakikisha anauwa kila mtu duniani na kumpeleka kuzimu; ambako anaishi yeye, majini, malaika waovu, wana wa Mungu waliotumwa na Mungu kuja duniani kufundisha watu utukufu lakini wakaasi na Mungu akawalaani (au Wanefili) pamoja na nguva. Nguva ni uzao wa Wanefili na samaki wa baharini na malaika wauvu na wanapatikana zaidi katika Bahari ya Atlantiki, ambako mkuu wake ni Malkia wa Pwani, na katika Bahari ya Hindi ambako mkuu wake ni Malkia wa Bahari ya Hindi. Chini ya Bahari ya Hindi ndipo yalipo makao makuu ya ufalme wa giza hapa duniani.
— Enock Maregesi
atlantic-oceanbahari-ya-atlantikibahari-ya-hindi