Peter, naomba nitubu kosa. Mimi si mtoto wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Ni mtoto wa Rais wa Meksiko. Lisa ni mtoto wa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali,†Debbie alisema akitabasamu.
“Hata mimi nilijua ulikuwa ukinidanganya. Lakini mbona Rais wa Meksiko haitwi Patrocinio Abrego?†Murphy aliuliza.
“Utamaduni wa Meksiko ni tofauti kidogo na tamaduni zingine,†Debbie alijibu baada ya kurusha nywele nyuma kuona vizuri. “Hapa, watu wengi hawatumii majina ya pili ya baba zao. Hutumia jina la kwanza la mama la pili la baba; ndiyo maana Wameksiko wengi wana majina matatu. Kwa upande wangu, Patrocinio ni jina la baba yake mama yangu na Abrego ni jina la babu yake mama yangu – kwa sababu za kiusalama.
— Enock Maregesi
attorney-generalbabababu