Kabla ya kukata roho mapigo ya kasi ya moyo aliyoyapata Yesu kutokana na mshtuko wa hipovolimia, pia yalisababisha maji kujikusanya katika vifuko vya maji au ute kandokando ya moyo na kandokando ya mapafu. Mkusanyiko huu wa maji kandokando ya moyo hujulikana kama ‘pericardial effusion’ na mkusanyiko wa maji kandokando ya mapafu hujulikana kama ‘pleural effusion’. Hii ndiyo maana baada ya Yesu kukata roho, na askari wa Kirumi kurusha mkuki katika ubavu wake, baada ya kutoboa mapafu na moyo, damu na maji vilitoka katika mbavu za Yesu kama Yohana alivyorekodi katika Injili yake. Mapafu ya Yesu na tumbo la Yesu vilijaa damu na maji. Mkuki ulivyotupwa maji yalitoka katika mapafu ya Yesu na katika tumbo la Yesu, na katika utando unaozunguka moyo wa Yesu, kutokana na kupasuka kwa moyo.

Related Quotes