Kuamini (mbali na imani, ambayo ni nia ya kujua kisichoweza kujulikana) ni kwa ajili ya vitu usivyoweza kuvielezea. Unaamini kwamba siku moja dawa ya UKIMWI au saratani itapatikana mahali fulani, ilhali huwezi kufanya majaribio ya kisayansi kulithibitisha hilo. Unaweza kusubiri hata miaka mia, lakini kama bado dawa haijapatikana, unaweza kusubiri hata miaka mingine mia. Kuamini ni kujifanya kujua (na mara nyingi kujifanya kujua ni uongo) na kuamini hakuhitaji maarifa. Kujua kunahitaji maarifa na ni kuamini unakoweza kukuthibitisha. Ukiniuliza kama simu yangu ipo mfukoni nitakwambia ndiyo ipo, kwa sababu nitaingiza mkono mfukoni na kuitoa na kuiona. Siamini kama ipo mfukoni, najua.
— Enock Maregesi
aidsbelievecancer