Majina ya vitabu yanapaswa kuchaguliwa kwa mantiki na kwa makini ya hali ya juu mno, kwa sababu ni miongoni mwa vitu vya kwanza watu wanavyoviona na kuvisoma. Watu wakivutiwa na jina la kitabu, au mwandishi; kitu cha pili watakachovutiwa kuangalia ni dibaji, kusudi wasome muhtasari wa kitabu kizima. Kwa hiyo dibaji inapaswa iandikwe kwa mantiki na kwa makini ileile iliyotumika katika kuchagua jina la kitabu. Lengo la jina la kitabu na dibaji ni kuishawishi hadhira kusoma kitabu na kukifurahia.
— Enock Maregesi
audienceaudiencesbook