Debbie alilia. Alilia kwa nguvu zake zote. Alijua tayari alishampoteza Murphy na yote yale huenda alisababisha yeye. Bila kujuana na Vijana wa Tume huenda wasingepigwa. Debbie Hakukata tamaa. Alikumbuka kitu halafu akamwita dereva. Alimwomba dereva amkimbize Roma Notre haraka ilivyowezekana. Alidhani alijua majambazi walikokuwa wakikimbilia na kuna kitu alitaka kufanya. Dereva akamkubalia na kuondoka kuelekea Roma Notre. Njiani Debbie hakuacha kulia. Aliwaza alivyompoteza Marciano, akawaza kumpoteza na Murphy. Jibu alilolipata ni kumwokoa Murphy kwa gharama yoyote ile.

Related Quotes

Murphy. Sina mbinu zozote za kujikinga kama unavyojua; mbali na mafunzo ya FBI. Baada ya kumrusha nyoka wa Lisa nywele zilinisisimka. Wazo la kukimbia likaja ghafla. Kukimbia hata hivyo nikashindwa kwa kuhofu huenda wangeniona. Hivyo, nikarudi nyuma ya nyumba na kupanda mti na kujificha huko. Bunduki zilipolia, nilijua wamekuua. Ila kitu kimoja kikanishangaza: mashambulizi hayakuonekana kukoma. Kitu hicho kikanipa nguvu kwamba huenda hujafa na ulikuwa ukipambana nao. Kimya kilipotokea nilijua umewashinda nguvu, kitu ambacho kumbe kilikuwa kweli. Nilipokutafuta baadaye lakini bila kukuona kutokana na kukurukakara za maadui niliamua kwenda katika gari ili nije na gari kama mgeni, nikitegemea waniruhusu kuingia ili nipate hakika kama wamekuua au bado uko hai. Wasingenifanya chochote. Kimaajabu, niliposhuka katika mti ili nikimbie katika gari, niliona gari ikija kwa kasi. Kuangalia vizuri nikakuta ni Ferrari, halafu nikashangaa nani anaendesha gari ya Lisa!”
Murphy alitabasamu tena na kuendelea kusikiliza.
“Sijui moyo wangu ulikuwaje. Sikuogopa tena! Badala yake nilikaza mwendo na kuendelea kuifuata huku nikipata wazo hapohapo kwamba mtu aliyekuwemo akiendesha hakuwa adui. Adui angeingia katika gari na kunisubiri aniteke nyara.” Debbie alitulia.
“Ulihisi ni mimi?” Murphy aliuliza.
“Nilihisi ni mtu tu mwema amekuja kunisaidia ... au mwizi wa gari. Hata hivyo, baadaye nilijua ni wewe na furaha yangu yote ilirudi.
Enock Maregesi
aliveautomobilebunduki